Muhammad Hamada amesisitiza
kwamba, jinai mtawalia za wavamizi na walowezi wa Kizayuni dhidi ya
msikiti wa al-Aqswa zinazidi kuimarisha moyo wa muqawama na mapambano
dhidi ya maghasibu.
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imekuwa ikisisitiza mara kwa mara kuwa, msikiti wa al-Aqswa utaendelea kubakia kuwa mstari mwekundu wa Waislamu na kwamba, kila mkono wenye lengo la kuuvunjia heshima msikiti huo utakatwa.
Israel inashadidisha vitendo vyake haramu na kubadili muundo wa kijiografia na kijamii wa mji wa Quds sambamba na kufuta utambulisho na utamaduni wa Kiarabu kupitia mipango yake ya ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na miundomsingi inayohusiana na vitongoji hivyo ikiwemo na kujenga barabara na njia ya chini kwa chini.
Hujuma za walowezi wa Kizayuni dhidi ya msikiti wa al-Aqswa vimekithiri zaidi baada ya kuingia madarakani serikali yenye misimamo mikali ya Benjamin Netanyahu ambayo imekuwa ikionyesha chuki za wazi wazi dhidi ya Wapalestina na maeneo yao matakatifu.
Vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu huko Palestina vinafanyika katika hali ambayo, viongozi wa nchi za Kiarabu na jamii ya kimataifa wameendelea kunyamaza kimya na kutochukua hatua zozote za maana za kukabiliana na vitendo hivyo vinavyokinzana na utu na ubinadamu.
342/